ads

Breaking News

Davido na Wizkid watajwa kuwania kipengele kimoja ‘2014 MOBO Awards’, hakuna msanii wa Afrika Mashariki


wizkid-davido

Wasanii wenye ushindani mkubwa nchini Nigeria Davido na Wizkid, wametajwa kuwania tuzo za MOBO Awards (Music Of Black Origin) wote wakiwa kwenye kipengele kimoja cha ‘Best African Act’.

David na Wizkid wanachuana na wasanii wengine wa Nigeria katika kipengele hicho ambao ni Yemi Alade, Tiwa Savage na Dr. Sid.
Wengine wanaowania tuzo za MOBO kwenye kipengele hicho ni Mafikizolo na DJ Clock wa Afrika Kusini, Afrikan Boy wa UK mwenye asili ya Nigeria, Fuse ODG na Mista Silva Waghana waishio UK.
Hakuna msanii yeyote wa Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo hizo za MOBO zinazotarajiwa kutolewa October 22, 2014 jijini London.
Tuzo za MOBO zilianzishwa 1996 na Kanya King na Andy Ruffell kwaajili ya kutambua wasanii wenye makabila mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wanaofanya muziki wa watu weusi. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka nchini Uingereza.

No comments