Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro,
katika kipengele cha msanii bora anayechipukia, Young Killer aka Msodoki
amesema kuwa kitendo cha msanii mkongwe, Banana Zorro kumshirikisha kwenye
wimbo wake ‘Samehe Sahau’ kimemfanya apate moyo wa kujituma zaidi katika kazi
zake.
Young Killer amesema kuwa Banana ambaye pia ameshirikishwa kwenye
wimbo wa rapper huyo ‘Umebadilika’ alimpigia simu kumuomba ashiriki kwenye
wimbo huo uliorekodiwa kwenye studio za Dully Syles, 4.12. Alidai kuwa Banana
hajamshirikisha kwenye wimbo wake kwakuwa naye alimshirikisha kwenye
‘Umebadilika’ bali ameona kuwa rapper huyo kutoka Mwanza anaweza kuandika kitu
kizuri kuupendezesha wimbo huo.
“Kikubwa nilisikijia furaha kwanza kufanya kazi pia kwa Dully akiwa kama
producer na pia ngoma niliipenda na nilienjoy kufanya,” amesema Young Killer.
“Nasikia furaha sana kwakuwa wasanii ambao tumekuja sasa hivi ni wengi toka
kizazi cha akina Banana lakini kwakuwa kanichagua mimi naamini ni heshima.”
Rapper huyo amedai kuwa ‘Samehe Sahau’ ni wimbo wenye ujumbe muhimu kwa watu
wa rika zote na tayari wameshashoot video yake.
No comments