Diamond amtaja muimbaji wa kike wa Tanzania anayemkubali zaidi
Diamond Platnumz amemtaja Vanessa Mdee kama muimbaji anayemkubali zaidi na ambaye anaona atafika mbali zaidi.
Diamond amesema hata jukwaani, Vanessa ni msanii anayejituma sana.
“Unajua wasanii wa kike wote wa hapa nyumbani ninawakubali ila namkubali sana Vanessa. Na hata nikikutana naye huwa namwambia kuwa ‘Vanessa unanipa imani sana kuwa tuna mwanamuziki wa kike ambaye naona kabisa anabadilika kila siku na anajituma sana hata akiwa kwenye stage’. Unaona kabisa ana juhudi zaidi maana Vanessa alikuwa akiimba kizungu sana lakini kila siku zinavyoenda anabadilika na anaelewa nini anafanya sio mtu wa kujitoa fahamu,” alisema.
“Kwahiyo nina imani ipo siku tutaona msanii wa kike kutoka Tanzania anafanya vizuri. Kwahiyo Vanessa namkubali sana na nina imani atafika mbali, ni mfano mzuri sana pia na kwa wengine kujituma zaidi na kuwa wabunifu wa kazi.”
No comments