Tuzo aliyojipa H.Baba ‘Mtumbuizaji Bora’ ni diss kwa Diamond Platnumz?
Pamoja na H.Baba kuwahi kudai kuwa hana tena beef na Diamond Platnumz, kuna kila ishara kuwa mafahari hao wawili bado hawawezi kukaa kwenye zizi moja.
Kama umesahau, wacha tukukumbushe; Wasanii hao wawili wamewahi kuingia kwenye beef zito baada ya H.Baba kumtuhumu Diamond amemuibia wimbo wake ‘Sitaki Kulewa’.H.Baba akipokea tuzo alizoandaa mwenyewe
So, Jumamosi iliyopita, H.Baba na mke wake, Flora Mvungi waliandaa tuzo zao wenyewe ambazo tofauti na vile wengi wanavyodhani, tuzo hizo zilikuwa serious kabisa kwa kuhusisha watu muhimu kwenye tasnia ya burudani Tanzania, waandishi wa habari na pia kutolewa trophy na fedha taslimu kwa washindi.
H.Baba alijipa tuzo ya ‘Mtumbuizaji Bora’ na tunafahamu kuwa Diamond Platnumz ni mshindi wa kipengele cha ‘Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki’ kwenye tuzo za KTMA 2013. H.Baba anataka title yake kutoka kwa Diamond?
Diamond alishinda tuzo 7 mwaka jana kwenye KTMA ikiwemo ya Mtumbuizaji Bora
Haya ni maneno aliyosema wakati akipokea tuzo hiyo:
“Tuzo hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,” alisema muimbaji huyo. “Mimi nina tuzo ya East Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo moja kwa sababu ya nini nimeshatangaza naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala sivuti bangi. Mimi sivuti sigara wala sinywi pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio halali yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote ajitokeze huyo msanii alipwe pesa mimi nita- perform bure na awadhihirishie watanzania kwamba yeye ni mkali ya stage Tanzania.
Kama ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila mimi kama H.Baba nitaperform bure na nitakuja peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa sababu kuna Kiswahili fasaha ambacho kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji bora na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji bora, wengine ni watumbuizaji bora. Kwanini nasema watumbuizaji bora kwa sababu msanii yeye mwenyewe hajiwezi mpaka awe na watu wakucheza naye, ila mimi binafsi najiweza kwa sababu mimi mwenyewe ninaweza fanya kazi na ikaeleweka.
Ndiyo maana ya hii tuzo niliyopata leo. Ninaowatambua walikuwa watumbuizaji na ninawaheshimu mpaka leo nawataja watu wawili, kuna Mr Nice kuna TID (Top In Dar ) hao ndo watu wanaweza kusimama kwenye show na kuburudisha na watu wakasema asante.”
No comments