Video: Kim Kardashian ashambuliwa na shabiki, mlinzi amsaidia
Mwanamitindo huyo alivamiwa ghafla na shabiki mmoja kumrukia na kumvuta kwa nguvu kiasi cha kutaka kumuangusha chini sekunde chache baada ya kushuka kwenye gari lake.
Kwa bahati nzuri mlinzi wake aliwahi kumshikilia asifike ardhini huku akionekana kujaa uoga kufuatia tukio hilo.
Kwa mujibu wa video iliyowekwa na TMZ, mama yake Kim Kardashian, Kris Jenner alishuka kwenye gari haraka na kwa mshituko alipiga kelele akisema ‘stop it’ kabla walinzi hawajamdhibiti mwanaume huyo na kumtoa katika eneo hilo.
TMZ imemtaja mtu aliyetekeleza tukio hilo kuwa ni Vitalii Sediuk ambaye ni plankster (mchekeshaji anaefanya utani wa kweli wa kushitukiza kwa mastaa) Ukraine aliyewahi kumshambulia pia Brad Pitt, Leo DiCaprio Will Smith.
No comments