VIDEO :::Rais Obama alaani mauaji ya PILI YA mwandishi Mwingine wa habari
Rais wa Marekani Barack Obama
amesema kuwa Marekani haitatishwa na mauaji wa mwandishi mwingine wa
habari Mmarekani na kundi la Islamic state.
Akiongea na waandishi wa habari nchini Astonia
Rais obama amesema kuwa mauaji hayo yanaichochea Marekani kukabiliana
ziani na magaidiVideo hiyo iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa Islamic State inamuonyesha mwanamme aliyejifunika uso wake na kisu mkononi akisimama juu ya Sotlof.
Nchini uingereza waziri mkuu David Cameron ameongoza mkutano wa kamati ya dharura ya serikali kujalidili jinsi itakavyojibu tishio la kutaka kumuua mateka raia wa uingereza.
Kwenye video hiyo mwanamgambo aliyejifunika uso na anayezungumza kiingereza anayaonya mataifa ya kigeni na kuyataka kusitisha harakati zao dhidi ya kundi la Islamic State.
Sotlof ni mwandishi wa pili wa Mmarekani kuuawa kwa kukatwa kichwa ndani ya mwezi mmoja baada ya mwandishi mwingine James Foly kuuawa kwa kukatwa kichwa mwezi uliopota na wanamgambo wa ISIS.
No comments