ads

Breaking News

Amber Rose kaitaja sababu nyingine ya kuachana na Wiz Khalifa, picha ya ushahidi iko hapa pia


Amber1
Kuvunjika kwa ndoa ya mastaa Amber Rose na Wiz Khalifa kumeendelea kuchukua nafasi kwenye headlines za dunia na hii ni baada ya Amber kutaja chanzo mojawapo cha kuvunjika kwa uhusiano huo.

Kwenye interview ya Radio Amber amesema kingine kilichomkasirisha ni kuona Wiz anawaendekeza warembo flani wawili mapacha ambao inaaminika amekua akijihusisha nao kimapenzi.
Amber amesema alipenda kuiokoa ndoa yake ili waendelee kuwa pamoja lakini anaeonekana kukataa kuendelea kuwa kwenye ndoa ni Wiz mwenyewe, Amber anasema hata taarifa za mwanzoni kwamba walitengana siku nyingi kabla ya kutaka talaka zilikua za uongo…. hakufanya maamuzi yao sababu alitaka kuiokoa ndoa yake.
amber 2
Amber amemshutumu Wiz kwa kutoka kimapenzi na hawa mapacha kwenye hii picha hapa chini…
amber 3

No comments