Ndoa ya Tiwa Savage na mme wake yadaiwa kuwa matatani, ampiga chini mmewe kama meneja
Mdudu wa kuvunja mahusiano na ndoa za mastaa amehamia Afrika, ambapo kuna tetesi kuwa ndoa ya muimbaji wa ‘Eminado’ Tiwa Savage wa Nigeria na mume wake aitwaye Tunji aka ‘Tee Billz’ inaelekea kuvunjika, ikiwa ni miezi mitano tu toka wawe mme na mke.
Miongoni mwa sababu zinazoongeza uzito wa tetesi hizo ni baada ya Tiwa Savage kumpiga chini mmewe kama meneja wake, na kuajiri meneja mpya aitwaye Emeka aka Meka Millions. Tee Billz ndiye aliyekuwa akisimamia kazi za Tiwa.
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Sahara Reporters kuwa ndoa ya Tiwa na Tee huenda ikavunjika sababu Tiwa hafurahii tena mapenzi ya mmewe.
Inadaiwa kuwa Tiwa aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji 2Face Idibia, kabla hawajaachana na 2Face kumuoa msichana mwingine aitwaye Annie Macaulay ambaye ndiye mkewe. Pia inasemekana Annie Macaulay (mke wa 2Face) aliwahi kuwa mpenzi wa Tee Billz kabla hawajaachaana na Tee kumuoa Tiwa.
Hivyo inasemekana kuwa Tiwa alikubali kwa haraka kuolewa na Tee ili kumlipizia 2Face na Tee alimuoa Tiwa kumlipizia Idibia.
No comments