ads

Breaking News

Album ya Flavour ‘Thankful’ yauza kopi milioni 1 ndani ya siku 5!

Untitled
Album mpya ya msanii wa Nigeria, Flavour iitwayo Thankful iliyotoka November 14, imeuza kopi milioni moja hadi sasa, kwa mujibu wa mitandao ya Nigeria.
Album hiyo ilitoka bila promo wala matangazo yoyote, kama alivyofanya Beyonce.
Kwa mujibu wa kampuni ya Obaino Music, inayohusika katika uuzaji wa album hiyo yenye nyimbo 21, hadi jana Jumatano walikuwa wameshauza kopi milioni 1 za kwanza. Kampuni hiyo imesema kwa jinsi msanii huyo anavyopendwa, album hiyo itauza kopi nyingi zaidi.
Album hiyo imewashirikisha wasanii mbalimbali wakiwemo M.I, Phyno, Wande Coal na Chidinma.

No comments