Young Killer asema hajakutana na vikwazo toka aanze kujisimamia mwenyewe
Msodoki ambaye wiki iliyopita ameachia single mpya ’13’ aliyomshirikisha Fid Q, amesema anajaribu kujisimamia mwenyewe japo hajakutana na vikwazo vyovyote hadi sasa.
“Mimi ni msimamizi mwenyewe, najisimamia mwenyewe, najaribu” alisema Msodoki kupitia Power Jams ya EA Radio Ijumaa iliyopita.
“Hakuna kikwazo chochote ambacho kinatokea, lakini kikubwa nachojifunza ni kwamba hata ikitokea siku kwa mfano tungekuwa katika management labda Mona hayupo na natakiwa nifanye tukio kwa muda huo ina maana mwenyewe ningeweza kufight”. Aliongeza.
Video ya ‘13’ iliyoongozwa na Nisher inatarajiwa kutoka November 13.
No comments