ads

Breaking News

Khloe Kardashian aupuuzia ushauri wa ndugu zake waliomtaka aachane na French Montana

Khloe Kardashian Celebrates Her 30th Birthday At TAO Las Vegas
Khloe Kardashian ameutupilia mbali ushauri aliopewa na ndugu zake waliotaka aachane na boyfriend wake French Montana kwa madai kuwa anamsaliti.

Kwa mujibu wa TMZ, Khloe hajali chochote kama mpenzi wake ana wanawake wengine au laa.
Mtandao huo umedai kuwa Khloe ameupuuzia ushauri wa familia yake, na amesema kuwa yeye anakula raha na hakuna kikubwa anachokitarajia hivyo waachane na ‘biashara yake’ ya uhusiano wake na French Montana.
TMZ iliripoti kuwa ndugu zake na Khloe walimuonya aachane na French kwa madai kuwa hivi Karibuni alipokuwa Dubai, alimtumia Kim Kardashian waliyekuwa pamoja kwenye safari hiyo, ili ionekane kuwa muda wote wakiwa huko alikuwa naye karibu huku wanafamilia wakidai kuwa ukweli ni kwamba French alikua na mwanamke mwingine.

No comments