ads

Breaking News

Mashabiki wa Alikiba wamrarua Babalevo


10832257_1508273096099411_1279430605_n
Babalevo amewachokoza nyuki na sasa anauguza maumivu.
Rapper huyo amejikuta akipokea matusi ya kila aina kutoka kwa mashabiki wa Alikiba waliochukizwa na ujumbe wale wa dhihaka kwa mfalme wao, hitmaker wa ‘Mwana’.Pengine akitafuta njia ya kuongeza ucheshi kwenye ujumbe wake wa pongezi kwa Diamond kufuatia ushindi wake kwenye tuzo za Channel O, Jumamosi hii, Babalevo alipost picha ya kitanzi na kuandika:
Ally kiba naomba uingie mwenyewe coz umeyataka mwenyewe.. sungura ulikuwa umesha mkamata eti umemuachia kiboya boya sasa kumkamata tena itaghalimu miaka mitano… Sisi wote Tupo kwenye Sanaa ila nguvu tunazidiana ndomana ally nilikuona mkombozi Wetu coz we ni fundi muziki.. Inakuwa je unajianguaha kwenye kumi na nane?????? Badala ya kufunga unategemea penati… Ona sasa refa kapeta… Na kufanya Kwa sasa tukubali bwana @diamondplatnum ni #KIBOKO japo alikwapua Ka aidia kangu na ndo kanakompa mijituzo.. Ila nime hands up… Ally kiba na diamond wote ni ma home boy kutoka KIGOMA ila mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni… Hii ni kick kuna mtu yeyote mwenye snea?”
Ujumbe huo ulisababisha hasira isiyo kifani kutoka kwa mashabiki wa Alikiba ambao kama wangeweza kumuona live muda huo, huenda angechezea kichapo kikali.
“Hv ww unahc unaweza mfkia Aly kiba cku moja kichwa kikubwa akil tope nngekuona wa mana ungechochea kuelewana kwao bt ndo kwanza unaongea pumba kutafta tension au ndo kujpendekeza kwa dai kwa style hyo hv unaelewa unachoimbaga au unafoka tu na ushkuru kigoma oll star ilkutoa wngne tulkua ht hatukujui tulza mshono uctafte kick kwa nguvu,” aliandika mmoja.
“Hahaaaaa anaangaika huyooo maana hata mwanangu nikimuuliza hakujui. Pyeeeeeeeeeee.unaacha kusifia tunzo iliopatikana nikwawantanzania unaanza kutaja majina yawatu.hata Wewe siunaimba kwann jamani kwann umseme mwenzio.jitahidi nawewe boya Wewe,” aliandika mwingine.
Mwigine aliandika: Sura yenyewe imekomaa kama ngozi ya goti mm sijawahi kukuelewa hata cku moja kwenye kazi zako yaani nilishakusahau kama na ww unaimba kama vp rudi kigoma ukavue dagaa kama mziki umekushinda waache watoto kina kiba wenye mji wao mtu mkubea akili huna jipangee.”

Baada ya kuona risasi aliyoipiga imemrudia mwenyewe, Babalevo alijaribu kuweka mambo sawa kwa kupost picha nyingine akiwa na Alikiba na kuandika:
“Ally kiba eeeeeeeeeeeeeeeeee niokoe babaaaaaaaa…… mashabiki wako watanimalizaaaaaaaaaa…. Mi nilikuwa kwenye maswala ya kutoa maoni tu babaaa……coz @diamondplatnumz ametunyooooooshaaaaaa…..sasa we ndo #mkombozi tuliye kuchagua tuokoe babaaaaaaa…… Kachukua tuzo tatu si unajua anatumia nguvu za GIZAAAA?
Hapana chezea mashabiki wa ‘Mwana Dar es Salaam’

No comments