ads

Breaking News

Nicki Minaj alitoa mimba akiwa na miaka 15, mwanae angekuwa na miaka 16 sasa

Nicki Minaj ameamua kuzungumza masuala yake binafsi kwenye album yake, The Pinkprint itakayotoka hivi karibuni.
Kwenye wimbo wake mpya, All Things Go uliotayarishwa na Boi-1da, Vinylz, na Allen Ritter na kuandikwa na Ester Dean, Nicki mwenye miaka 31 sasa, anarap kuhusu kutoa ujauzito akiwa na miaka 15.
“My child with Aaron would have been 16, any minute/ So in some ways I feel like Caiah is the both of them/ It’s like he’s Caiah’s little angel, looking over him,” anarap.
Katika album hiyo, wasanii walioshirikishwa ni pamoja na Beyoncé, Lil Wayne, Drake, Chris Brown, Ariana Grande, Meek Mill, Skylar Grey, Jeremih na wengine.

No comments