ads

Breaking News

Young Killer: Wimbo niliowashirikisha Linah, Roma na Dimpoz sijaifanya kuwa official kwasababu tayari watu walishaisikia


Young Killer ameachia video mpya wiki hii ya wimbo uitwao ‘Mungu Baba’ aliowashirikisha Ommy Dimpoz, Linah na Roma, na huenda ukawa unajiuliza kama hiyo ndio official single yake mpya baada ya ‘13’ ama laa.

Msodoki ameiambia Bongo5 kuwa ‘Mungu Baba’ sio wimbo ramsi kama single mpya baada ya ‘Kumi Na Tatu’ aliyofanya na Fid Q.
“Sio official ndio maana sijaipeleka redioni. Hiyo ngoma mara ya kwanza nilishagaifanya, ila nilipata comments za watu kibao ebana ile ngoma mbona ni kali sana afu kama hukuiachiaga redioni yaani kama sikuitendea haki kui release. Kwahiyo ili kuwaridhisha wale watu ikabidi niifanyie video, na kuifanyia video yule mtu ambaye mara ya kwanza niliimba nae video alikuwa hayupo alikuwa Moshi na hapatikani ndo nikamchkua Linah nikamuweka akapiga ile chorus.”
Rapper huyo ameelezea pia jinsi ilivyokuwa mpaka Roma na Ommy Dimpoz wakahusika kwenye wimbo huo.
“Nikaipeleka Tongwe pale kwenda kufanyiwa mastering, Roma alikuwepo pale Tongwe ndo akawekea ile outro, baada ya hapo nikaichukua nikawa nataka kuiachia. Siku moja nilikua kwa Man Water nikakutana na Ommy Dimpoz pale baada ya kuonana na Ommy tukasema kwanini hatujawahi kupiga kazi, nikamwambia sio ishu basi nipigie hata Intro halafu ngoma ingine tutakayofanya official mimi na wewe hata itakuwa siku nyingine, ndo akawa amenipigia Intro, kwahiyo ndo nikawa nimeipata picha nzima ya hiyo ngoma.”
Hata hivyo Msodoki amesema kuwa inaweza kuchezwa redioni kwa sababu anaamini ni ngoma kali.
“Hii hata redioni hata wakitaka kupiga nitawaruhusu tu wapige kwasababu ni ngoma ambayo iko katika mahadhi mazuri na ni ngoma inayoweza ikawa hit song, sema sijaifanya kuwa official kwasababu tayari watu walishaisikia.”
Young Killer ameongeza kuwa single rasmi ambayo amefanya kwa Man Water ataiachia siku si nyingi.

No comments