DJ rasmi wa Jay Z, Young Guru kuwasha moto Dar, Jumamosi
Jiji la Dar es Salaam Jumamosi hii litapokea ugeni mkubwa kutoka kwa engineer wa muziki aliyeshinda tuzo za Grammy, Gimel Keaton maarufu kama Young Guru kutoka Marekani. Young Guru ni DJ rasmi wa rapper Jay Z.
DJ huyo maarufu, anayeheshimika na aliyepewa jina la ‘The Sound of New York’, atawarusha wakazi wa Dar kwenye kiota cha Club Rouge Jumamosi hii.
Young Guru huzunguka na Jay Z kwenye ziara zake na anafahamika kwa uwezo mkubwa wa kufanya mixing za album za wasanii na ameshahusika kwenye zaidi ya album 10 zikiwemo za mastaa kama Beyonce, Alicia Keys, Kanye West, Rihanna na Ludacris.
Guru atatumbuiza nyimbo za mahadhi mbalimbali zikiwemo Hip hop na R&B, Electro na mengine
No comments