Ray wa Bongo Movie akanusha kujichubua
Msanii wa filamu, Vicent Kigosi maarufu kama Ray amekanusha madai kuwa anajichubua.
Ray ameiambia Bongo5 kuwa anasikitishwa na watu wanaodai kuwa anajichubua bila kujua kuwa mtu akiwa na maisha mazuri anaweza kubadilika.
“Kwanza sijichubui, tatizo unajua baadhi ya watanzania wengi, hawaelewi mimi sijichubui, ila maisha yamebadilika,” amesema. “Unajua unapokuwa na maisha magumu ya kwanza, unaposhindwa kujikimu, kujinunulia nguo, yaani kufanya unachokitaka kwa muda unaoutaka, unakuwa mweusi kwa sababu huna hela ya kujikimu, sasa unapopata pesa kidogo ya kujikimu, unapokuwa na maisha mazuri , kwako kuna AC, kwenye gari yako kuna AC, hupati jua huwezi kuwa mweusi,” amesisitiza.
“Pia ukishakuwa star lazima muonekano wako uwe tofauti kidogo ili uwe tofauti kidogo. Hawa wanaoona mimi najichubua labla wanaona vibaya! Mimi sijichubui na waache waendelee
kuzungumza kwa sababu mtanzania huwezi kumzuia kuzungumza.”
No comments