The Rock ameweka wazi sababu za yeye kuacha mchezo wa mieleka…
Dwayne Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, movie producer na mchezaji mieleka kutoka Marekani aliejitengenezea jina kubwa kwenye mieleka na kufanya apate shavu kubwa kwenye movie za action Hollywood, Marekani.
The Rock alichukuwa time na kufanya interview na gazeti la Marekani Esquire na kuongelea mambo mengi ikiwemo sababu zilizomfanya aingie kwenye tasnia ya uwigizaji pamoja na mafanikio yake binafsi. The Rock alikuwa na haya ya kusema:
Kuhama kwenye mieleka kwenda kwenye uwigizaji:“Baada ya kufanikiwa kwenye mieleka, nilihamasika kujabiru uwigizaji wa movie za action, na nimefika hapa nilipo kwa kutumia nidhamu niliojinfunza kwenye mieleka, kujenga ukaribu na watu kwenye industry, na kujiunga na madarasa ya kuigiza”.
Kama anapendelea uwigizaji zaidi kuliko mieleka:“Mieleka ni mpenzi wangu wa kwanza, lakini kwenye uwigizaji kuna upendo tofauti ambao unaniruhusu mimi kugusa watu kupitia sanaa nyingine na pia kutengeneza hela ndefu zaidi, movie zinanifundisha mambo mengi sana ambayo nisingeweza kuyajua mwanzoni”.
No comments