Ne-Yo athibitisha kuwa anakuja Kenya kwenye Coke Studio Africa
Muimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo amethibitisha kuwa anakuja nchini Kenya hivi karibuni kwaajili ya kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa.
Siku chache baada ya taarifa kusambaa kuwa Ne-Yo ndiye msanii wa kimataifa atakayeungana na mastaa wa Afrika katika kipindi hicho mwaka huu, ametumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuthibitisha ujio wake.
Hii ni mara ya pili Ne-Yo anarudi Afrika katika kipindi cha muda mfupi. July 18, 2015 alitumbuiza kwenye tuzo za
MTV MAMA huko Durban, Afrika Kusini.
No comments