ads

Breaking News

Alicia Keyz ampa shavu Wizkid la kutumbuiza kwenye hafla yake ya ‘Keep a Child Alive’

Miezi miwili iliyopita Mastaa wa Marekani wakiwemo, Alicia Keyz na mume wake Swizz Beatz walipost kwenye mitandao video waki enjoy wimbo wa Wizkid ‘Ojuelegba’ ikiwa ni ishara kuwa wameukubali na kumkubali mwimbaji pia.
Wizkid2
Sasa Alicia Keyz amempa shavu staa huyo wa Nigeria, Wizkid kutumbuiza kwenye hafla ya kampeni yake ya ‘Keep a Child Alive ’ itakayofanyika November 5 kwenye jiji la New York.
Alicia Keyz na Chris Rock ndio watakuwa host wa hafla hiyo ambayo itakuwa pia na wasanii wengine ambao watatangazwa baadae.
‘Keep a Child Alive’ ilianzishwa na Alicia Keyz mwaka 2003 ikiwa ni kampeni yenye lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa watoto.

No comments