Diamond adai Tiffah amemfanya awe na ‘discipline’
Baba Tiffah, Diamond Platnumz amesema ameamua kuishi maisha ya kimaadili ili mtoto wake akikua asikutane na vitu vya ajabu.
Mshindi huyo wa tuzo tatu za Afrimma, ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM kuwa sio vizuri mwanae akikua aje akutane na picha chafu za baba yake.
“Sasa hivi nakuwa nazingatia sana maisha,” anasema. “Naiogopa kesho kuliko nilivyokuwa naogopa mwanzo. Pia kuna vitu fulani vya drama drama nimeamua kuvipunguza, naona vikienda vikikutana na mwanangu vitamchanganya,” aliongeza.
“Sio picha nzuri mwanangu akutane na picha ya baba yake anamtia denda demu. Kuna matukio fulani niliyokuwa nayafanya ya kinyama ambayo siwezi kuyafanya tena kwa sababu kiukweli binti yangu akiona atasema bad.”
No comments