Khloe Kardashian na Lamar Odom wafuta kesi yao ya talaka ili kuipa ndoa nafasi ya pili
Kwa mujibu wa TMZ, mwanasheria wa Khloe aitwaye Laura Wasser Jumatano Oct 20 alienda kwa hakimu kuomba kusitisha kesi hiyo huku wote wakiwa wamesaini hati ya kukubali kufuta kesi ya kusitisha ndoa hiyo, na jaji alifanya kama walivyoomba.
Lamar (35) na Khloe (31) walifunga ndoa mwaka 2009 na kutengana miaka minne baadae. Khloe alifungua kesi ya kudai talaka December 2013.
No comments