ads

Breaking News

Angelina Jolie: Mimi na Brad Pitt tuna matatizo kama wanandoa wengine

Mastaa nao wapo kama sisi tu.
bradjelina_2980307b
Angelina Jolie alizungumzia maisha na mume wake Brad Pitt Jumapili ya Nov. 8, na kuweka wazi kuwa mastaa hao nao wana wakati wa shida na raha kama watu wengine kwenye uhusiano.

“Mimi na Brad tuna matatizo kama wanandoa wengine wowote,” Jolie, 40, aliliambia gazeti la The Telegraph wakati akipromote filamu yake mpya, By the Sea. “Tuna siku ambazo hujikasirisha vibaya sana lakini matatizo kwenye filamu hii sio yetu wenyewe.”
Filamu hiyo iliyoongozwa na Jolie na kuchezwa na wao wenyewe inaonesha story ya wanandoa wanaopitia majaribu. Wawili hao wamewahi kuigiza pamoja kwenye filamu ya mwaka 2005, Mr. & Mrs. Smith.
Alisema awali wakati wanafanya kazi kwa pamoja ilikuwa tofauti kwakuwa walikuwa hawafamiani sana na walikuwa vijana na walidhani kuigiza kwenye By the Sea ingekuwa rahisi lakini haijawa hivyo.
Wawili hao walishoot video hiyo huko Malta muda mfupi baada ya kufunga ndoa August 2014 nchini Ufaransa.

No comments