Filamu mpya ya James Bond, Spectre yazinduliwa Dar
Mastaa mbalimbali
nchini mwishoni mwa wiki hii walijumuika katika uzinduzi wa filamu mpya
ya James Bond, Spectre uliofanyika Cape Town Fish Market jijini Dar es
Salaam.

Uzinduzi wa filamu hiyo iliyoigizwa na muigizaji wa Uingereza Daniel Craig kama James Bond, uliratibiwa na kampuni ya QWAY International.
Pamoja na Fish Market, filamu hiyo ilizinduliwa kwenye majumba mengine ya sinema nchini na duniani kote.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo mwakilishi wa kampuni ya QWAY International, Tanya Mulamula, alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia filamu hiyo mpya hasa kwa kuzingatia kuwa filamu za James Bond ni maarufu sana duniani.
“Baada ya hapa filamu hii sasa itaanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema hapa nchini,” alisema Tanya.

No comments