AGNESS MASOGANGE AHOJIWA UWANJA WA NDEGE DAR KWA ZAIDI YA MASAA 10
Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana
na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza
kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika
Kusini.
Nzowa alisema baada ya kuhojiwa, Masogange aliruhusiwa na kwamba yupo huru, ameachiwa bila masharti yoyote.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi
Selemani naye alithibitisha kuhojiwa kwa msanii huyo akisema: “Hapa kuna
kikosi kazi, kila mmoja alimhoji kwa wakati wake lakini kwa upande wa
polisi tulimpekua na kumhoji lakini tumemwachia.”
Kamanda Selemani alisema Masogange alianza kuhojiwa juzi saa mbili usiku hadi jana saa nne asubuhi.
Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo,
Masogange alikana akisema kwa kifupi na kukata simu: “Hilo unalosema
siyo kweli na sipo tayari kuzungumzia hilo… Siwezi kuzungumza na chombo
cha habari kwa sasa, shida yako nini?”
Masogange alitawala vyombo mbalimbali vya habari
nchini katikati ya mwaka jana baada ya kukamatwa Afrika Kusini akiwa na
nduguye Melisa Edward wakiwa na ‘mzigo’ wa dawa hizo zenye thamani zaidi
ya Sh6.8 bilioni.
Wasichana hao walinaswa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Nzowa alisema jana kuwa katika mahojiano hayo
walimuuliza kuhusiana na ushahidi alioutoa huko Afrika Kusini kuwa dawa
hizo za kulevya alipewa na mtu kutoka JNIA.
“Ni kweli tulikuwa tunamuhoji Masogange ili
atueleze mtu gani aliyempa crystal methamphetamine kama alivyodai kuwa
amepewa na mtu wa hapa JNIA,” alisema Nzowa.
Katika mahojiano hayo, Nzowa alidai kuwa Masogange
alidai kuwa alipewa dawa hizo na mtu ambaye hamfahamu kwa jina lakini
anaikumbuka sura yake.
Alisema baadaye walikwenda eneo ambalo walipeana
dawa hizo na mtu asiyemjua jina lake kwa ajili ya kuweza kumtambua kama
alikuwapo eneo hilo.
“Pia tulimuhoji kutaka kujua alikwenda Afrika Kusini kufanya nini, kwa sababu ipi, alimfuata nani na alifikia wapi,” alisema Nzowa.
“Pia tulimuhoji kutaka kujua alikwenda Afrika Kusini kufanya nini, kwa sababu ipi, alimfuata nani na alifikia wapi,” alisema Nzowa.
No comments