Makundi ya kislamu yanayoshikilia baadhi ya maeneo nchini
Iraq na Syria yamemua mwandishi wa habari, raia wa Marekani, James Foley,
yakieleza kwamba ni kujibu mashambulizi ya Marekani, ambayo ilianzisha
hivi karibuni dhidi ya ngome za wapiganaji wa makundi hayo.
James Foley alitekwa nyara tangu miaka miwili iliyopita nchini
Syria. Makundi hayo ya kislamu yametishia kuua raia mwengine wa
Marekani, ambayo yanamshikilia.
Foley ameoneshwa katika mkanda wa video akiuawa kwa kuchinjwa na
mmoja wa wapiganaji hao wa kislamu ambaye amekua ameficha uso, huko
akitishia kuua mwanahabari mwengine kutoka Marekani, ambaye pia
ameoneshwa katika mkanda huo wa video unaodumu dakika tano.
Mpiganaji huyo amesema mwandishi huyo wa Marekani atauawa kama jinsi
alivyouawa Foley, iwapo Barack Obama hatositisha harakati zake za
kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kislamu nchini Iraq. Jeshi
la Marekani linaendelea na mashambulizi dhidi ya makundi hayo ya
kislamu katika mji wa Tikrit, baada ya makundi hayo kupoteza eneo muhimu
la Mossoul.
James Foley ni mwandishi wa habari mwenye uzowefu mkubwa, ambaye
alifanya kazi yake wakati wa vita vya Afghanistan na nchini Iraq. Foley
aliwahi kukamatwa mateka pia kwa muda wa majuma 6 nchini Libya.
Familia ya mwandishi huyo wa habari imethibitisha kifo chake, huku
Marekani ikijizuia kutoa taarifa yoyote inayohusiana na kifo hicho.
Hayo yakijiri, jeshi la anga la Marekani limeanzisha mashambulizi ya
anga katika mji wa Tikrit. Mashambulizi hayo ni ya pili baada ya
kuwatimua wapiganaji wa makundi ya kislamu katika eneo mhimu kunako
patikana bwawa linalozalisha umeme wa kiwango kikubwa nchini Iraq katika
jimbo la Mossoul.
Hata hivo wapiganaji hao wanaonekana wana mafunzo ya kutosha na wana
silaha za kisasa kuliko majeshi ya Iraq, kwani baada ya jeshi la Iraq na
wapiganaji wa kikurdi kuteka eneo la Chichine kusini magharibi mwa Iraq
wakisaidiwa na jeshi la anga la Iraq, wanajeshi hao na wapiganaji wa
kikurdi wameanza kujiondoa katika eneo hilo.
Iraq : mwandishi wa habari, raia wa Marekani achinjwa
Reviewed by peacethepresident
on
August 20, 2014
Rating: 5
No comments