ads

Breaking News

KIKONGWE WA MIAKA 80 AISHI KWA KULA UDONGO

 

Katika hali ya kushangaza na kusikitisha sana, kikongwe mmoja aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu.Kikongwe huyo alikutwa na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani  zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo

No comments