NATISHA SANA: WAPI TWAELEKEA TANZANIA?! AMKATA KICHWA MDOGO WAKE APATE UTAJIRI!
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamng’ang’ania
mfanyabiashara maarufu wa Wilaya ya Mvomero, Johnson Damian Mkude (39)
akituhumiwa kumkata kichwa mdogo wake wa kuzaliwa, Mathias kisha
kuondoka nacho kwenda kwa mganga kwa kile kilichodaiwa ni kufanyiwa dawa
ili awe bilionea, mkasa wote huu hapa. Tukio hilo ambalo kwa sasa ndiyo gumzo mkoani hapa lilijiri usiku wa Agosti 3, mwaka huu katika
mashamba ya Kata ya Mlali ambapo ndugu wa marehemu waliokuwa wakimsaka
ndugu yao walifanikiwa kuona kiwiliwili Agosti 6, mwaka huu.
MWILI WAZIKWA KATIKA SHAMBA LA MTU
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na
kushuhudia kiwiliwili kikiwa kimeharibika vibaya. Ilibidi baba wa
marehemu, mzee Damian Mathias Mkude (63) amwombe mmiliki wa shamba hilo
lililopo kwenye Kijiji cha Mbalala, Kata ya Mlali kumzika mwanaye hapo
ambapo alikubali.
BABA WA MAREHEMU
Akizungumzia tukio hilo kwa uchungu, baba wa marehemu mzee Mkude alisema:”Mwezi mmoja kabla ya tukio,
Johnson alinichonganisha na Mathias, nakiri hadi marehemu anakufa
nilikuwa sina uhusiano naye mzuri kutokana na maneno aliyoniambia kaka
yake
No comments