ads

Breaking News

Picha: AY na wasanii wengine wa Afrika watumbuiza mjini Washington DC

10570052_1445816099017153_1929229684_nRapper Ambwene Yessaya ambaye yupo jijini Washington DC, Marekani pamoja na wasanii wengine, leo wametumbuiza mbele ya viongozi mbalimbali wa Marekani na Africa. Show hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Newseum mjini DC.


“Jana (juzi) ilikuwa ni tour ya kwenda white house na nini, kuelezewa mambo ya mule ndani na baadaye usiku tukafanya rehearsal mpaka usiku wa manane,” AY aliiambia Bongo5 jana. “Leo (jana) sasa ndo kila kitu, watu tunakutana kwaajili ya kujadili na baada ya hapo tutafanya show leo usiku. Chochote kitakachojadiliwa nitawajuza. Kesho pia ni kuna mkutano mwingine, pia viongozi mbalimbali marais wako hapa wanawasili na mwenyeji mkuu yuko hapa, kesho pia kutakuwa kuna dinner white house,” alisema.

No comments