Sporah ashambuliwa baada ya kupost video akimwagiwa ndoo ya maji ya barafu kuunga mkono ‘Ice bucket Challenge’
Mtangazaji wa kipindi cha ‘The Sporah Show’ kinachoruka kupitia Clouds
Tv, Sporah Njau ameshambuliwa na mashabiki baada ya kupost video ya
inayomuonesha akimwagiwa ndoo ya maji ya barafu, kama ishara ya
kushiriki kampeni ya ‘Ice bucket Challenge’ inayofanywa Marekani
kuhamasisha kuchangia utafiti juu ya ugonjwa wa Amyotrophic lateral
sclerosis (ALS).