ads

Breaking News

Member wa Navy Kenzo ajitoa kundini


Member wa Navy Kenzo, Weestar amejiondoa katika kundi hilo na kujiunga na kampuni mpya ya kusimamia kazi za wasanii inayoitwa Ngoma Entertainment.
Msanii huyo ameamua kufanya muziki na watu wamfahamu kama Weestar na sio kama member wa tatu wa kundi la Navy Kenzo.
Hivi sasa Navy Kenzo imebaki na wasanii wawili ambao ni wapenzi, Nahreel na Aika.
Ameamua kuwa huu ni muda wa watu kumfahamu kama Weestar na sio kama member wa tatu wa Navy Kenzo. Anaamini kila msanii ana sauti yake na wajibu wake wa kuwapa watu kile Mungu alichompatia. Single yake ya kwanza kama msanii anayejitegemea inaitwa ‘Naiye’ na inatoka Ijumaa hii kwenye vituo vya redio.” Wamesema Ngoma Entertainment kwenye maelezo yao.

No comments