Video ya ‘Mr. Nay’ yamfanya Nay wa Mitego aitwe na mama yake mzazi
Nay wa Mitego msanii wa bongofleva ambae amethibitisha kwamba Mama yake mzazi amemuita na kutaka kujua kilichoonekana kwenye video yake mpya ya ‘Mr. Nay’ aliyoifanya Kenya kinamaanisha nini.
Nay ambae kabla ya kufanikiwa kimuziki aliwahi kuwa kinyozi wakati bado akisoma sekondari,amesema mama yake mzazi amemuita nyumbani September 2 2014 kutaka kujua kinachoendelea sababu alichoona na anachoambiwa na watu kimemfanya apate wasiwasi mkubwa.
Nay anasema ‘mimi nafanya kitu kutokana na idea ambazo huwa zinatoka kichwani mwangu, nafikiri watu wameona ni video kubwa nzuri na kali…. sijawahi kufanya video kali kama hii ambayo kidogo inataka kuniletea shida ila sio kitu kibaya kwangu’
No comments