Mr Blue aliacha uigizaji baada ya kugundua anapoteza tu muda
sasa hivi kaonekani kwenye tasnia hiyo.
Blue ambaye alionekana kwenye filamu ya Pretty Teacher na House Boy, ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa, baada ya kuingia kwenye filamu na akagundua hakuna maslahi aliamua kuachana na kazi hiyo.
“Nilikuwa najaribu zali na kuangalia upepo umekaaje kwa mashabiki, ingawa fani hii nilianza tangu nipo shule,” alisema Blue.
Aliongeza, “Nilipima maji kati ya muziki na filamu kipi kinalipa zaidi, nikagundua muziki ulikuwa juu zaidi, nikaingia kwa miguu yote na kweli niliona faida nyingi kwa muda mfupi sana,” aliongeza.
No comments