Nagharamia ya Christian Bella na Alikiba haitoki bila video
Christian Bella amesema wimbo aliofanya na Alikiba ‘Nagharamia’ utachelewa kuachiwa kwakuwa walikubaliana kuanza na video.
Bella amesema wameamua kuonjesha tu wimbo huo ili kuwatoa hofu mashabiki wanaoisubiria kazi hiyo kuwathibitisha kuwa ni kweli wameshaurekodi.
“Tulikubaliana kushoot video ndio tutoe kazi,” amesema Belle.
“Kwahiyo hatujapata nafasi ya kushoot video. Labda tutaondoka Jumatatu kwenda kushoot video tumejipanga sijui kama kutakuwa na mabadiliko yoyote. Watu wameisubiria sana, kwangu mimi nilikuwa nashindwa hata kuongelea. Unajua ukifanya kolabo unakuta mwenzako yupo busy, akipata nafasi na wewe unakuwa busy,” alikiambia kipindi XXL kupitia Clouds FM.
“Kwahiyo kutoa teaser hiyo ni kuwafanya watu waelewe kazi ipo na wasione kama ilikuwa longo longo. Ila sijapromise watu kwamba inatoka lini, kwa sababu tunapishana sana kuhusu ratiba, tunashindwa kupata nafasi. Kwahiyo kusema kweli sijui tutaitoa lini. Kwahiyo ninachoomba mimi ni tupate nafasi tukafanye video ikifanyika ndio tutajua.”

No comments