Barnaba afanya kazi na msanii mwingine wa Uganda, ‘Kleyah’
Wawili hao wanarekodi wimbo uitwao ‘Msobe Msobe katika studio za High Table zinazomilikiwa na Barnaba.
Barnaba ameiambia Bongo5, “Kleyah alinitafuta kupitia simu alipewa namba yangu kupitia kituo kimoja hivi cha redio. Ni msanii ambaye mwenye uwezo mkubwa sana na sikutegemea kama msanii kama huyu anaweza kunitafuta maana nilimfutilia nikaangalia biography yake ipo vizuri, lakini aliniamini na ndio maana tukafanya kazi. Nimemuimbisha Kiswahili humo ndani vizuri ameimba.”
Kleyah ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kuchukua elimu yake ya juu katika masuala ya mawasiliano katika chuo cha Phoenix nchini Marekani.
Kwa sasa Kleyah anaishi nchini Tanzania akiwa anatarajia kukamilisha masomo yake ya utawala wa kimataifa (Degree in
International Management).
Pamoja na kusoma, msanii huyo yupo chini ya usimamizi mkufunzi wa masuala ya sauti, Luigi Tamburi pamoja na Mzungu
Kichaa. Nyimbo zake za awali ni pamoja na ‘Lovers Eyes’ na ‘Don’t Sly me’ zilizotayarishwa na Ogopa Djs wa Kenya.
No comments