Mshukiwa wa Boko Haram akamatwa baada ya shambulizi la Bomu jijini Abuja
Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtu mmoja anayetuhumiwa
kutekeleza shambulizi katika duka la jumla jijini Abuja siku ya Jumatano
na kusababisha vifo vya watu 21 na wengine kujeruhiwa.
Shambulizi hilo lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram
lilitokea katika duka la Emab Plaza saa 10 jioni wakati wakaazi wa jiji
hilo walipokuwa wanafanya manunuzi ya bidhaa kabla ya kwenda nyumbani.Msemaji wa polisi nchini humo Frank Mba amethibitisha kukamatwa kwa mshukiwa mmoja, na kuongeza kuwa watu waliojeruhiwa ni 17.
Kundi la kigaidi la Boko Haram limekuwa likitishia kuendeleza mashambulizi zaidi nchini humo wakati huu, jeshi likiendelea na Operesheni ya kuwasaka wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na kundi hilo.
Mwezi Aprili mwaka huu, kundi la Boko Haram lilivamia kituo cha basi cha Nyanya na kutekeleza watu 75 na baadaye kukatokea na shambulizi lingine papo hapo na kusababisha watu 19 kupoteza maisha.
Juma hili, Boko Haram liliripotiwa kuwateka zaidi ya wanawake na wasichana 80 katika jimbo la Borno na kuwapeleka kusikojulikana.
Boko Haram inasema iko tayari kuwaachilia wasichana hao ikiwa serikali ya Nigeria itawaachilia wanachama wake, suala ambalo serikali ya Nigeria imekataa
No comments