LIVE! MAMA AMSHIKA UCHAWI KIKONGWE HUYU,ADAI KAUA MTOTO WAKE KICHAWI
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo
No comments