ads

Breaking News

Diamond Vs Ali Kiba : Nay wa Mitego atamani kutembeza kipigo kikali kukomesha (Audio)

Ushindani kati ya Diamond na Ali Kiba ambao siku zote mimi nauita ‘ushindani usio rasmi’ huku wengine wakiutafsiri kama ‘beef’ umetengeneza mitazamo tofauti kati ya wadau wa muziki Tanzania.
Hivi karibuni, G-Lover alitoa mtazamo wake kuhusu tofauti iliyopo kati yao huku akimpa credit kila mmoja.
Akiongea na Fadhili Haule  katika Sunrise ya 100.5 Times Fm, Nay wa Mitego yeye ameeleza jinsi asivyopenda kabisa malumbano yanayoendelea kudai kuwa angekuwa na uwezo angetembeza kipigo heavy.
“Ningekuwa na uwezo wa kuwapiga wote ambao yaani wanaendelea huu mchezo uliopo, nafikiri ningewapiga na ningewafunga ningekuwa na amri hiyo.” Nay wa Mitego ameiambia Sunrise.
“Coz unajua kuna watu wanatengeneza hivi vitu, wanataka kuwatia watu stress. Wanataka watu ifike time waje wauane. Kuna beef tunaona zinakuwaga beef tu za kawaida. Lakini huu mchezo wa Ali Kiba na Diamond ni Mchezo ambao naona kama watu wanaoufanya uwe serious sana. Mimi sipendi nachukia.” Ameongeza rapper huyo wa ‘Itafahamika’.
Amewashauri Ali Kiba na Diamond kuachana kabisa na kinachoendelezwa kati yao na kuendelea na muziki kwa kuwa itafikia hatua mbaya ambayo wataumizana na kushindwa kufanya muzik

No comments