Kanye West kumtengenezea mwanae North pete ya ndoa, sasa
Kwa mujibu wa mtandao wa HollywoodLife, Kanye anataka kuwa mtu wa kwanza kumvisha pete hiyo kidoleni kwake. Kanye atamvisha mwanae pete hiyo ya almasi wakati huu akiwa na mwaka mmoja tu.
“Yupo kwenye mchakato wa kutengenezea pete ya almasi ya aina yake kwaajili ya kuvaa kwenye kidole chake cha ndoa,” chanzo kimoja kimeuambia mtandao huo. “Muite chizi, lakini hivyo ndivyo anavyotaka kufanya.”
“Hajali, atakuwa mwanaume wa kwanza kumvisha pete binti yake. Anasubiri mpaka mwanae awe mkubwa kidogo na atamwambia Lorraine kuitengeneza iendee kidole chake.”
Lorraine ni Lorraine Schwartz, mtengezaji wa vidani aliyetengeneza pete ya ndoa ya Kim Kardashian.
No comments